Chama cha AKP chapoteza ushawishi Uturuki

Kura zikihesabiwa Uturuki

Huku kura nyingi zikiwa zishahesabiwa katika uchaguzi mkuu wa Uturuki, chama tawala cha AKP kinaonekana kupoteza idadi kubwa ya wabunge wake.

Matokeo yanaonyesha chama hicho kimeshinda kwa asilimia arobaini na mbili ya kura, huku kikiwa na upungufu wa viti kumi na nne kuweza kuunda serikali.

Huku kile kinachoungwa mkono na wakurd cha HDP kikivuka asilimia kumi kwa kupata viti takriban themanini hivyo kuweza kuingia bungeni kwa mara ya kwanza.

Iwapo itathibitishwa, matokeo haya yanaashiria mwisho wa utawala wa miaka kumi na tatu wa chama cha AKP hali itakayokwaza mipango ya rais Erdogan ya kumpa rais madaraka zaidi.

Baada ya kupiga kura yake katikati mwa Uturuki katika mji wa Konya, waziri mkuu Ahmed Davutoglu aliongea na waandishi wa habari, na kuwaeleza kwamba"natarajia mema kwa nchi yangu na watu wangu. Leo niko hapa kama waziri mkuu kwa hiyo nina jukumu. Siku ya leo ni ishara ya imani ya nchi yetu, kwa hiyo nataka kusema asanteni nyote ambao mmeshiriki katika uchaguzi wa bila kujali uamuzi wenu."
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company