Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry alirejea Vienna Ijumaa kwa ajili ya duru ya mwisho ya mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano ya kimataifa yenye nguvu juu ya program ya nyuklia ya Iran
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry
Afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya marekani amesema wapatanishi wanaojaribu kufikia makubaliano katika program ya nyuklia ya iran wanaweza wasifanikishe kazi yao ifikapo muda uliopangwa wa Juni 30 lakini wanatarajia kukamilisha.
Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry alirejea Vienna Ijumaa kwa ajili ya duru ya mwisho ya mazungumzo yenye lengo la kufikia makubaliano ya kimataifa yenye nguvu juu ya program ya nyuklia ya Iran.
Mara mkataba huo utakapokamilika vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran vitaondolewa.
Katika matamshi yake ya hadharani Jumatano Kerry alisema wairani huenda wasione maana kamili ya hatua zitakazokubalika , katika sehemu ya makubaliano ya awali yanayojulikana kama “ mpango wa awali wa makubaliano” yaliyofikiwa April mwaka huu.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago