WATU watatu wamefariki dunia katika Kijiji cha Kalagu kwenye mwambao mwa Ziwa Tanganyika Wilaya ya Kigoma Vijijini kutokana na mlipuko wa kipindupindi huku wengine 10 wakiwa wamelazwa katika zahanati ya Gungu.
Akizungumza na chanzo cha habari Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Leonard Subi, alisema mpaka jana kulikuwa na wagonjwa 10 waliolazwa katika Zahanati ya Mwakizega ya wilayani Uvinza na watatu wamefariki dunia.
Dk. Subi alisema ugonjwa huo umelipuka kwa wananchi wanaoishi mwambao wa Ziwa Tanganyika kutokana na kuwapo raia wa kigeni kutoka nchi ya jirani ya Burundi ambao wanakuja nao.
Aliwaomba wananchi kuchukua tahadhari kutokana na ugonjwa huo kwa kuchemsha maji ya kunywa, kunawa mikono na kula chakula cha moto.
Idara ya afya ya mkoa wamejipanga kuweka mikakati ya kupambana na ugonjwa huo na kuhakikisha maji yote yanawekewa dawa kabla hayajafika kwa watumiaji, alisema.
"Ninawaomba wananchi waendelee kuchukua tahadhali kutokana na mlipuko huu wa kipindupindu ambao ni hatari… naomba wananchi wahakikishe wanaweka mazingira katika hali ya usafi na waache tabia ya kula kula hivyo,” alisema Dk. Subi.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago