Kama fedha kwa ajili ya ujenzi zimepatikana, serikali inatarajia angalau miaka mitano ya kazi ya kukarabati nchi ya Nepal. Picha zizopigwa katika Bhaktapur tarehe 5 Juni mwaka 2015.
REUTERS/Navesh Chitrakar
Na RFI
Nepal inaandaa Alhamisi Juni 25 mkutano wa kimataifa wa wafadhili, miezi miwili tu baada ya moja ya matetemeko zaidi ambayo yaliikumba nchi hiyo.
Nchi 41, ikiwa ni pamoja na nchi saba za Asia Kusini zinazojumuika katika shirika la Ushirikiano wa Kikanda na taasisi 22 za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Tume ya Ulaya, Umoja wa Mataifa na Benki kuu ya Dunia, walioalikwa. Changamoto ni nyingi.
Miezi miwili iliyopita, siku hadi siku, Nepal ilikumbwa na moja ya majanga mabaya ya asili katika historia yake. Matetemeko mawili makubwa yaliwaua zaidi ya watu 8,700 na kuharibu miundombinu. Takribani watu milioni 2 walipoteza mali zao.
Kama maisha yameanza kuchukua polepole mkondo wake, maelfu ya watu wanaendelea kuishi katika makaazi ya muda na hali inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na ujio wa vimbunga. Changamoto ni kubwa. Kwa mujibu wa viongozi wa Kathmandu, nchi inahitaji " misaada mikubwa ya kimataifa ", kwa sababu inasadikiwa kuwa janga hilo liligharimu dola bilioni 10, sawa na nusu ya pato la ndani la taifa kwa mwaka.
Kwa hiyo Nepal inatarajia kuongeza angalau kati ya dola bilioni 6 na 7 ya msaada kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, miundombinu, maeneo ya kitamaduni na shule.
Misaada ya kimataifa iliyotolewa mpaka sasa imefikia dola milioni 150. Pesa hiyo ni ndogo kwa kujenga upya na kukarabati nchi, ikiwa ni pamoja na maeneo muhimu ya shughuli mbalimbali, hususan kilimo na utalii ambavyo viliteketezwa. Viongozi wa Nepal wamesema itachukua angalau miaka mitano ya ujenzi wa nchi hiyo.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago