MWENGE WA UHURU WAFUNGUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA KIBEDYA WILAYANI GAIRO.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Ndugu Juma Khatib Chum akifungua mradi wa maji wa Kijiji cha Kibedya Wilayani Gairo.

Kiongozi wsa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ndugu Juma Chum pamoja na mwezake wakiwatwisha ndoo za maji Pelis Taolo na Jesca Msange wa Kijiji cha Kibedya muda mfupi baada ya mradi wa maji wa Kibedya kufunguliwa.

Mwenge wa uhuru ambao kwa sasa uko Mkoani Morogoro, umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji uliogharimu shilingi 555,227,710.40 na unatazamiwa kuwapatia maji safi na salama wananchi 10,534 ambao ni wakazi wa kijiji cha Kibedya Wilayani Gairo.

Mwenge huo ambao umeingia siku yake ya pili, tangu kuwasili Mkoani Morogoro ukitokea Mkoani Tanga, na kukimbizwa Wilaya ya Mvomero, Leo ukiwa Wilayani Gairo umefungua mradi wa maji wenye matenki mawili yenye jumla ya lita za ujazo 180,000.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Bw. Juma Khatib Chum, muda mfupi kabla kuufungua, ilielezwa kuwa mradi wa maji wa Kibedya uliibuliwa na wananchi na kuingizwa kwenye program ya Serikali ya miradi ya maji ya vijiji kumi Wilayani Gairo.
Mradi wa Maji wa Kibedya umejengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mpango wa maendeleo ya Sekta ya Maji, na wananchi kuchangia ardhi ulipojengwa mradi huo yenye thamani ya shilingi 1,500,000,.00.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa lengo mahsusa la mradi huo ni kuwapatia wananchi wa Kijiji cha Kibedya maji safi na salama hali itakayochangia kuboresha maisha yao kwa kupata muda wa kutosha kufanya shughuli nyingine za kiuchumi badala ya kutumia muda huo kutafuta maji.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Khatib Chum baada ya kuufungua, mradi huo, aliwataka wananchi wa Kijiji cha kibedya kuuendeleza na kuutunza mradi huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu.
“ Ninawasihi wananchi wa Kijiji cha Kibedya kuendeleza na kutunza miundombinu ya mradi huu pamoja na vyanzo vyake vya maji ili mradi udumu kwa muda mrefu na kuja kunufaisha vizazi vingine vijavyo” alisema.
Mwenge wa uhuru leo umekimbizwa katika Wilaya ya Gairo ambapo umepitia jumla ya miradi ya maendeleo sita, yenye thamani ya shilingi, 905,071,355.40.
Hiyo ikiwa ni pamoja na mchanggo kutoka Serikali Kuu ni shilingi 715,390,635.40, mchango kutoka Halmashauri ya Gairo shilingi 7,578,720.00, nguvu za wananchi silingi 180,387,000.00 na wahisani walichangia shilingi 1,715,000.00.
Mwenge wa Uhuru kesho utakimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. (DK)
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company