![]() |
Talha Asmal Kijana mdogo raia ya Uingereza aliyejitoa mhanga |
Talha Asmal, mwenye umri wa miaka 17, alikuwa mmoja kati ya washambuliaji wanne wa kujilipua ambao walishambulia majeshi karibu na mtambo wa kusafisha mafuta kusini mwa Baiji.
Mitando ya mawasiliano ya kijamii inahusisha shambulio hilo na kundi la Islamic State (IS) anasema Asmal, gambaye anaitwa Abu Yusuf al-Britani, ambaye alishiriki katika shambulio hilo.
Familia yake wanasema walisononeshwa na habari hizo.
Asmal, kutoka Dewsbury, angekuwa Mwingereza kijana kuliko wote kufahamika katika mashambulio ya kujilipua. Kijana mwingine kutoka West Yorkshire, Hasib Hussein, alikuwa na umri wa miaka19 wakati alipojilipua katika basi la London katika shambulio la Julai 7,2005.
Talha Asmal alitoroka na kujiunga na Islamic State mwezi Marchi Taarifa iliyotolewa na familia ya Asmal inasema: "Talha alikuwa na upendo,mpole, anayejali na kijana mwenye bashasha.