Umoja wa katiba ya Watanzania (UKAWA) unaoundwa na vyama vinne vikuu vya upinzani nchini humo NCCR MAGEUZI, Chadema, CUF na NLD unaelekea kukumbana na changamoto katika maandalizi yao kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu nchini humo.
Akizungumza na VOA kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa alieleleza kwamba suala la ubinafsi limeshika kasi nchini humo na kuwataka wapinzani wafikirie kwa mapana na kuliweka pembeni suala hilo kwasababu urais ,ubunge ,uwakilishi au udiwani ni utumishi wa umma ni jambo la kujitoa mtu binafsi kwa ajili ya kutumikia wanyonge akiwataka wawe na sauti moja katika upande huo.
Kuhusu mpango wa kutoa mgombea wa urais kwa Umoja huo jambo ambalo lilikuwa na tetesi kuegemea Chadema ameeleza kwamba watakaa “kiutuzima” na kukubaliana kwamba nafasi si ya urais pekee, kuna nafasi nyingi za utumishi wa taifa na waangalie kwa mujibu wa sheria huyo mgombea urais anapatikana vipi na makamu wake anapatikana vipi , na sifa za rais kwa mujibu wa katiba na tume ya uchaguzi nchini Tanzania zinatekelezwa vipi na baada ya hapo kuna nafasi nyingi za utumishi wa taifa.
Kwa hiyo tetesi la swala la kuegemea Chadema amelitupilia mbali kuwa ni mambo ya majungu, fitna na kufarakanisha akiongeza kwamba walioko madarakani wasingependa wao wakaendelea kuwa na ushirikiano huo uliopo.