Umoja wa Ulaya kuwapa hifadhi wahamiaji

Boti yenye wakimbizi kutoka Tunisia ikiwasili kisiwa cha Lampedusa nchini Italia

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wakiendelea na kikao chao hadi usiku wa manane mjini Brussels wamekubaliana kuwahamisha maelfu ya wahamiaji ambao waliingia katika nchi za Italia na Ugiriki.

Mwenyekiti wa kikao hicho Donald Tusk amesema wahamiaji 40,000 watapelekwa katika mataifa mengine ya Ulaya katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Hata hivyo, hakutakuwa na mgawanyo wa lazima kwa nchi kuwapokea wahamiaji hao.

Mgogoro wa madeni ya Ugiriki pia ulizungumziwa katika kikao hicho. Ugiriki na wakopeshaji wake wa kimataifa bado hawajafikia muafaka baada ya mazungumzo ya Alhamisi.

Mapema, Bwana Tusk amezitaka nchi wnachama wa EU kugawana mzigo wa wahamiaji haram ambao wamevuka bahari ya Mediterani.

Takwimu mpya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR zinaonyesha wahamiaji 63,000 waliingia Ugiriki kwa njia ya bahari mwaka huu na wengine 62,000 waliingia nchini Italia. Viongozi hao pia wamekubali kuwapokea wakimbizi wengine 20,000 kutoka nje ya Umoja wa Ulaya.

Uingereza imejitoa katika mpango huo, ambapo mataifa ya Ulaya mashariki yamekataa kukubaliana na kugawana wahamiaji, kwa hiyo itabaki kuwa hiyari. Hatua ya nchi hizo imemwuudhi Waziri Mkuu wa Italia Matteo Renzi, ambaye amesema mpango huo ni mzuri.

Italia imeomba msaada zaidi kutoka washirika wake wa EU kushughulikia mzigo wa wahamiaji.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company