UN yaadhimisha miaka 70 ya uhai wake

Rwindi, Kivu Kaskazini, DR Congo: askari wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa kutoka India, Novemba 19 mwaka 2014.
Photo MONUSCO/Force
Na RFI
Ilikuwa Juni 26 mwaka 1945 katika mji wa San Francisco, wakati wawakilishi wa nchi 50 walitia saini kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa siku moja baada ya kupitishwa bila kupingwa.


Siku hiyo, rais wa Marekani Harry Truman alitangaza: "dunia inaweza kuanza kutafakari wakati ambapo binadamu wote wanaweza kuishi maisha mazuri ya watu waliyo huru watu".

Je Umoja wa Mataifa ni ndoto nzuri au mafanikio katika mahusiano ya kimataifa ? Kwa miaka 70 sasa, na hasa tangu kumalizika kwa vita baridi, mjadala umeendelea kuibuka.

Itakumbukwa kwamba ni miaka 70 sasa, Mkataba umejiwekea malengo ya kuusaidia ulimwengu katika masuala ya usalama na uheshimishwaji wa haki za binadamu hasa "Kudumisha amani na usalama wa kimataifa, kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, kufikia ushirikiano wa kimataifa katika kutatua matatizo ya kimataifa yanayohusiana na uchumi, jamii, utamaduni au ubinadamu ". Malengo mazuri yaliyo wazi ambayo hayakukabiliana na vita baridi kwa " usawa wa ugaidi ", muda mfupi baada ya kusaini mkataba mjini California.

Umoja wa Mataifa ulianzishwa katika kipindi kigumu. Ishara ya wazi ni matumizi ya kura ya turufu kwa Moscow na Washington, ambayo kwa miongo kadhaa iliathiri uamuzi kla uamzi wa Baraza la Usalama. Baada ya kubanwa katika nafasi yake kama mlinzi wa amani, Umoja wa Mataifa umekua sasa, baada ya kumalizika kwa ukoloni, jukwaa la nchi mpya kutoka Afrika na sauti kwa nchi ambazo zilikua zikiitwa za ulimwengu wa Tatu. Wakati huo, Umoja wa Mataifa ulipendekeza kuundwa kwa utaratibu mpya wa uchumi katika ngazi ya kimataifa.

Mipaka ya Umoja wa Mataifa

Kuanguka kwa Ukuta wa Berlin, na baadae kuvunjika kwa USSR, kulipelekea Umoja wa mataifa kuzindikana, kwani Baraza la Usalama halikua linabanwa tena na kura ya turufu ya nchi hizo mbili "zenye nguvu". Hivyo basi , nchi za dunia zilijikuta pia zinaunda Umoja wa Mataifa. Ilikuwa muamko wa haraka ambao ulisababisha kukuwa kwa migogoro, kwani mwaka 1990 George Bush alihitaji Umoja huo wa Mataifa kuunda muungano dhidi ya Saddam Hussein.

Na baadae kulitokea migogoro nchini Somalia, Bosnia, mauaji ya kimbari nchini Rwanda, mapambano dhidi ya ugaidi tangu mwaka 2001, Darfur, misimamo mikali ya kidini, Syria, Ukraine ...

Migogoro mingi ilionyesha mipaka ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na katika nyanja ya siasa (hata kama baadhi ya makatibu wake wakuu kama Boutros Boutros-Ghali na Kofi Annan walijaribu kuonysha kuwa pingamizi yeyote katika medani ya kimataifa), na kukosa uwezo wa kudumisha amani.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company