waandamana wakiwa uchi Uganda
Wanawake katika kijiji kimoja cha kazkazini mwa Uganda wamefanya maandamano wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kwa takriban miaka 10.
Wakati wa maandamano hayo ,mawaziri wa serikali na watafiti walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko Amuru.Maandamano
Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakaazi wakidai kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi ,mwanamke anapovua nguo na kusalia uchi ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa laana kwa mpinzani wake.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago