Mabalozi 110 wa CCM Monduli wahamia CHADEMA

Mabalozi wa mashina mia moja na kumi wa CCM,Mwenyekiti,Katibu kata, Wajumbe wa kamati ya siasa ya kata pamoja na Wenyeviti wa mitaa minne katika kata ya Monduli mjini mkoa Arusha wamehama CCM na kuhamia Chadema.

Tukio ilo limetokea Monduli mjini jana majira ya saa sita mchana wakati viongozi hao walipo kusanyika na kutoa kauli ya kuhama CCM na kuhamia Chadema huku wakisema chama cha Mapinduzi kinaongozwa kibabe na kimekosa mwelekeo.

Kwa upande wao wenyeviti wa serikali za mitaa,wajumbe wa nyumba kumi na katibu wa CCM kata ya Monduli Anna Erinest wameitaka jamii itambue kuwa hayo ni maamuzi yao binafsi na hayahusiki na shinikizo la mtu yoyote kama inavyo daiwa na baadhi ya watu kwamba kila wanaohama hudaiwa wameshinikizwa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company