![]() |
Meli kubwa ya mizigo yatia nanga bandari ya DSM |
Meli kubwa ya mizigo ya CLEMENS SCHLUTE yenye uwezo wa kubeba makasha 5500 mara moja imetia nanga bandari ya DSM kama ishara kuwa bandari hiyo inaweza kutumiwa na meli kubwa za mizigo duniani.
Mkurugenzi wa kitengo cha kutoa huduma za upakuaji makasha Bandarini - TICTS, DONALD TALAWA amesema meli hiyo imetoka Thailand na ujio wake utawavutia wafanyabiashara wa ndani na nje kuitumia bandari ya DSM kwa sababu gharama za usafirishaji mizigo zitapungua.