Bilal mgeni rasmi sherehe za Idd leo

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limetangaza kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za Idd El Hajj leo yanayofanyika kitaifa mkoani Mara ni Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal.

Bakwata ilieleza jana kuwa sherehe hizo zitafanyika katika mji wa Musoma na Idd itaswaliwa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mkendo, saa mbili asubuhi na Baraza la Idd saa nane mchana.

Sikukuu ya Idd el Hajj au Idd el-Adha inaadhimishwa baada ya kukamilika kwa ibada ya Hija, moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu ambapo kwa sasa mahujaji wako katika ibada hiyo nchini Saudi Arabia.

Mjini Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Idd, litakalofanyika Mkokotoni mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakary, swala ya Idd inatazamiwa kufanyika kitaifa katika Msikiti wa Mkokotoni na Baraza la Idd kufanyika katika Chuo cha Amali, Mkokotoni Unguja.

“Maandalizi ya swala ya Eid na Baraza la Eid yamekamilika ambapo kitaifa utafanyika katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkokotoni,” alisema Bakary.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company