CHAMA CHA SYRIZA CHASHINDA:UGIRIKI

Alexis Tsipras akishangilia ushindi Ugiriki
Chama cha mrengo wa kushoto nchini Ugiriki cha Alexis Tsipras kimerejea tena madarakani nchini humo baada ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi.

Kwa kura nyingi zilizopigwa, hazikuweza kutoa viti vya kutosha bungeni kwa chama hicho kuunda Serikali huku Waziri mkuu Tsipras akiwa tayari amekubali kuungana na mrengo wa kulia kuunda serikali.

Tsipras amesema kuwa Ugiriki ilikuwa na kipindi kigumu lakini waliweza kupigana ndani ya Ugiriki na hadi katika nchi za Jumuiya ya Ulaya na kwamba wataendelea na mapambano kuikwamua Ugiriki.

Kulikuwa na furaha miongoni mwa wafuasi wa chama hicho katika mji wa Athens.

Kiongozi wa chama cha New Conservative Vangelis Meimarakis amekubaliana na matokeo hayo,na kutoa tamko rasmi la kuunga mkono ushindi huo.

Akizungumza nje ya makao ya chama chake amesisitiza kuundwa serikali madhubuti.BBC
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company