Rais wa mpito nchini Burkina Faso Michel Kafando amesema kuwa amerudi mamlakani na uongozi wa raia kurudishwa takriban wiki moja baada ya mapinduzi.
Tangazo hilo lilijiri wakati ambapo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Gilbert Diendere alienda kuwakaribisha viongozi kadhaa wa Afrika ili kusimamia uhamisho wa madaraka.
Walinzi wake walikubali mkataba wa usiku kucha na jeshi la kawaida kutozua ghasia.
Waliahidi kurudi kambini huku jeshi likiondoka katika mji mkuu.
Walinzi hao wa rais ni watiifu kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Blaise Compaore ambaye aliliongoza taifa hilo kwa miaka mingi na kung'atuliwa mamlakani mwaka uliopita.
Walinzi hao walimweka jenerali Diendere kuwa kiongozi wa taifa hilo wiki iliopita kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini humo.
Walimzuia rais Kafando wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri siku ya jumatano.
''Raia wapendwa,mimi niko huru na nimerudi kuchukua uongozi. Serikali ya mpito imerudi mamlakani na imechukua madaraka'',bwana Kafando aliwaambia waandishi.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago