Serikali yaagiza shule zifungwe Kenya

Image copyrightothersImage captionWalimu wamekuwa wakiishinikiza serikali kuwalipa nyongeza ya mishahara ya asilimia 50 hadi 60

Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia Jumatatu huku mgomo wa walimu ukiendelea.

Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani.

Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.

Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT ameambia BBC kuwa tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.

Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule “zamani”.

Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo iwapo mgomo huo wa walimu, ambao umelemaza masomo muhula wa tatu, ni halali au la.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company