Taasisi ya Twaweza imetoa utafiti wake ambao inasema imefanya kwa wananchi wa Tanzania bara kutoka mikoa tofauti ya Tanzania.
Swali la kama uchaguzi ungefanyika leo, ungempigia kura mgombea wa chama gani? wanasema watu wamejibu kama ifuatavyo
CCM - 66%
CHADEMA - 22%
CUF - 1%
ACT wazalendo - 0%
UKAWA - 3%
Kingine - 6%
Hakuna jibu 2%
Utafiti huo uliotokana na kuhoji watu 1848 kutoka mikoa tofauti ya Tanzania bara, inasema iliwauliza wananchi hao: Ukimwacha Rais Kikwete, iwapo uchaguzi wa urais ungefanyika leo, ungemchagua nani?
...Majibu ya swali hilo TWAWEZA wanasema limejibiwa na wananchi hao kama ifuatavyo
Magufuli 65 %
Lowassa 25%
Mwingine 3%
Sijui/kataa jibu 7%
Akitangaza utafiti huo leo, Mkurugenzi mtendaji wa TWAWEZA, Aidan Eiyakuze amesema kwa upande wa ubunge, Utafiti huo unaonyesha kuwa CCM inaongeza kwa asilimia 60 na kufuatiwa na CHADEMA asilimia 26.
Takwimu zinaonyesha kwamba wananchi hawaelewi nafasi rasmi ya Ukawa
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago