Waziri Celina Kombani afariki dunia

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani amefariki Dunia kutokana na maradhi ya Saratani, na amefariki akiwa India ambako alienda kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kuhusu taratibu zinazofatia, nimeipata taarifa kutoka Ofisi za Bunge ambapo inaonesha mipango ya kusafirisha mwili wa Marehemu mpaka Dar es Salaam inafanyika na mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Dar Jumatatu September 28 2015, na baadae msiba utasafirishwa kupelekwa Mahenge Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mazishi.
    Marehemu Mama Celina Kombani amefariki akiwa na umri wa miaka 56 na alikuwa Waziri na pia Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki.

Mtandao huu unatoa pole kwa familia ya marehemu na taifa kwa ujumla kwa msiba huu.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company