Mgombea anayepewa nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi wa urais nchini Argentina, Daniel Scioli, akiwasalimu wafuasi wake baada ya kupiga kura, Oktoba 25, 2015, Buenos Aires.
AFP/AFP
Na RFI
Wananchi wa Argentina wamejitokeza kwa wingi kwa kupiga kura Jumapili hii Oktoba 25 na wamekua wakisubiri usiku wa Jumapili kuamkia Jumatano matokeo ya uchaguzi wa rais ili kujua kama mgombea kutoka mrengo wa kushoto, Daniel Scioli, ameshindakatika duru ya kwanza au mshindani mwenza kutoka chama cha kihafidhina Mauricio Macri, atamlazimisha kuingia katika duru ya pili.
Takriban wananchi Milioni thelathini na mbili kwa jumla ya milioni 41 wametakiwa kupiga muhuri wa sura ya kumi na mbili wa utawala wa Nestor (2003-2007) na Cristina Kirchner (2007-2015). Vituo vya kupigia kura vimefungwa saa 12:00 joni saa za Argentina (sawa na saa 3:00 usiku saa za kimataifa).
Ni vigumu kusema kwa uhakika kama Daniel Scioli atashinda katika duru ya kwanza au kama uchaguzi mwengine utapigwa tena Novemba 22. Zoezi la uhesabuji limeanza na matokeo yanatazamiwa kujulikana usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu wiki hii.
Nchini Argentina, inatosha tu kuwa na 45% ya kura katika duru ya kwanza, au tu 40% ikiwa tofauti na wa pili inafikia pointi 10.
Tangu mwaka 1973, Argentina ilipitisha kanuni ya uchaguzi wa urais kwa duru mbili, lakini chaguzi saba zilizoitishwa tangu mageuzi ziliamuliwa kufuatana na duru ya kwanza.
Mwaka 2003, Nestor Kirchner hakuwa na kura za kutosha ili kuepuka duru ya pili, lakini mshindani mwenza Carlos Menem alijiuzulu kabla pambano hilo. Kama uchaguzi huu wa nane wa urais utaingia katika duru ya pili, utakuwa wa kwanza.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago