Orodha ya wapiga kura katika kituo cha kupigia kura katika mji wa Brazzaville wakati wa kura ya maoni ya katiba nchini Congo-Brazzaville, Oktoba 25, 2015.
REUTERS/Roch Baku
Na RFI
Jumapili Oktoba 25, nchini Congo-Brazzaville, wananchi walitakiwa kupiga kura ya rasimu ya katiba mpya ambayo huenda ikamruhusu Rais Sassou Nguesso kuwania kwa mara nyingine uchaguzi wa uras wa mwaka 2016. Marekani iliomba kura hiyo ya maoni iahirishwe.
Umoja wa Ulaya umebaini kwamba " hali ya sasa hairuhusu uchaguzi huru na wa uwazi"nchini Congo-Brazzaville. Hata hivyo kura ya maoni imefanyika Jumapili Oktoba 25 katika hali ya taharuki wakati ambapo upinzani uliwataka wafuasi wake kususia kura hiyo ya maoni. Kura ya maoni ambayo haikua na shauku kubwa.
Vituo vya kupigia kura vimefungwa nchini Congo-Brazzaville, na haijajulikana kiwango cha watu walioshiriki zoezi hilo, lakini jambo moja ni la uhakika, zoezi la uhesabuji halitochukua muda mrefu. Saa 12 jioni, ni muda ambao ulipangwa vituo vyote vya kupigia kura kufungwa. Vituo karibu vyote katika manispaa kuu ya Brazzaville vilikua vimeshafungwa saa 12 jioni.
" Tumelazimika kufunga, kwa sababu tlikua hatuna wapiga kura na pia kwa ajili ya usalama ", afisa wa kituo kimoja cha kupigia kura cha kata ya Makélékélé, amesema kwa masharti ya kutotajwa. Hii ina maana kwamba katika sehemu hii ya mji inayodhibitiwa na upinzani, kura ya maoni imepigwa katika hali ya mvutano, huku maafisa wa vituo vya kupigia kura wakisubiri chini ya kua kali wapiga kura ambao hawakuweza kujitokeza.
Watu wameanza kujitokeza mchana
Wakazi wa maeneo haya wameitikia wito wa kususia zoezi hilo uliyotolewa na upinzani au tu waliacha kuonyesha uaminifu waokwa vyama vyao vya kisiasa? Ni vigumu kusema. Baadhi ya wakazi pia wangelipenda kupiga kura, lakini wamelaumu kuona hawakupata kadi za kupigia kura.
Kwingineko katika mji mkuu, zoezi hilo limeanza kwa hali ya wasiwasi pia, lakini mwishoni alaasiri foleni ndefu zimeonekana katika vituo mbalimbali vya kupigia kura. Kila mmoja amekua akipongeza namna zoezi hilo limefanyika. Kwa ujumla, wananchi wengi wa Congo waliojielekeza kupiga kura wamesisitiza umuhimu kwao kwa kushiriki zoezi hilo kama wajibu wao wa wananchi na wote wakiwa na matakwa sawa: kudumisha amani na kukomesha machafuko.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago