Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva imemtangaza Rasmi mgombea Urais wa CCM,Dr John Pombe Magufuli kuwa mshindi halali wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.
Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr magufuli amepata ushindi wa kura Milioni 8 ( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.45% huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu , Edward Lowassa (Chadema ) ambaye amepata jumla ya kura Milioni 6 ( 6,077,848 ) sawa na asilimia 39.97%
Dr Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu watakabidhiwa rasmi vyetu vya ushindi kesho saa nne asubuhi katika ukumbi wa hoteli ya Diamond Jubilee
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago