Kura zaanza kuhesabiwa katika vituo vya kupiga kura katika maeneo tofauti nchini

Baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika hapo saa 10 jioni, baadhi ya vituo vimeanza kuhesabu kura huku baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mbeya wakiipongeza


Baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika hapo saa 10 jioni, baadhi ya vituo vimeanza kuhesabu kura huku baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mbeya wakiipongeza Tume ya Uchaguzi ya Taifa –NEC- kwa maandalizi mazuri ya kufanikisha zoezi la upigaji kura licha ya kasoro ndogo zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo.

Wakizungumza na TBC kwa nyakati tofauti wamesema zoezi la upigaji kura kwa mwaka huu limekuwa na mwamko mkubwa kwa wananchi hali inayoonyesha wengi wana elimu ya uraia.

Nako mkoani Dar es Salaam, TBC ilitembelea baadhi ya vituo na kushuhudia polisi wakilinda vituo hivyo wakati kura zikiwa zinahesabiwa huku kukiwa na hali ya utulivu na wananchi kutokuwepo katika maeneo hayo.

Baadhi ya kasoro zilizojitokeza katika jiji la DSM ni kutokuwepo kw amajina ya wananchi katika daftari la kudumu la kupigia kura walilokuwa nalo wasimamizi wa uchaguzi katika kituo cha shule ya MUGABE jimbo la UBUNGO hali iliyowafanya wapiga kura katika kituo hicho kukaa mpaka wakati wa kuhesabu kura wakiwa wanasubiri kujua hatma yao.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company