![]() |
Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya uchaguzi -NEC RAMADHANI KAILIMA |
Akizungumza baada ya baadhi ya vituo kuhitimisha zoezi hilo KAILIMA amesema huko SUMBAWANGA watu wasiojulikana waliliteka nyara gari lilolobeba vifaa vya uchaguzi na kuliteketeza kwa moto wakati katika kata ya KIMARA wilayani KINONDONI wafanyakazi wamechana karatasi za kura kwa kudai malipo zaidi
Naye Mkurugenzi wa huduma za sheria wa NEC EMMANUEL KAWISHE amesema Tume itaendelea kusimamia sheria za uchaguzi
Tume ya taifa ya uchaguzi imetoa angalizo kuwa hakuna mtu yeyote anayetakiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi kuanzia ngazi ya udiwani hadi wa urais isipokuwa tume hiyo pekee.