
Viongozi wa Afrika wakiwa katika mkutano wa AU, Addis Ababa Ethiopia
Msemaji
wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Eri Kaneko, amesema kuwa suala la
Congo ni zito na kwamba mazungumzo bado yanaendelea, ingawa hakutoa
taarifa zaidi kuhusu uamuzi huo.
Ikiwa
leo ni siku ya pili na ya mwisho ya mkutano huo, masuala kadhaa hasa
yanayohusu migogoro iliyozikumba nchi za Afrika ikiwemo Mali, Sudan na
Sudan Kusini pamoja na Jamuhuri ya Kidemocrasia ya Congo yataendelea
kujadiliwa.
Pia
suala la kutafuta fedha na vifaa kutoka Umoja wa Mataifa kwa ajili ya
kuvisaidia vikosi maalumu vya Umoja wa Afrika nchini Mali, na kupambana
na wanamgambo wa Kiislamu.
Hapo
jana Pande zinazohusika katika mgogoro huo wa DRC zilitarajiwa kutia
saini mkataba wa amani lakini muda mfupi kabla ya tukio hilo, Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon akatangaza kuwa mazungumzo hayo
yamevunjika.
Habari
zinasema Afrika Kusini imegoma kuridhia mazungumzo hayo baada ya
kutoridhika na maelezo yaliyotolewa na pande zinazohusika na mazungumzo
hayo.
