ome Local General Watuhumiwa wa ukataji mkono wa albino wafikishwa mahakamani Watuhumiwa wa ukataji mkono wa albino wafikishwa mahakamani


Watuhumiwa watano wanaodaiwa kushiriki katika kitendo cha kumkata mkono Mlemavu wa ngozi Albino Maria Chambanenje
Watuhumiwa watano wanaodaiwa kushiriki katika kitendo cha kumkata mkono Mlemavu wa ngozi Albino Maria Chambanenje
Watuhumiwa watano wanaodaiwa kushiriki katika kitendo cha kumkata mkono Mlemavu wa ngozi Albino Maria Chambanenje wa kijiji cha Miangalua wilayani Sumbawanga wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi wilayani Sumbawanga kusomewa mashtaka yao.
Watuhumiwa  hao  wamefikishwa  mahakamani  baada  ya uchunguzi wa  jeshi  la  polisi  kubaini  walikuwa  na  mkono wa  Albino  huyo ambao walifukia ardhini   mara baada  ya kuukata. 
Watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi na kusomewa mashtaka yao huku wakitakiwa kutojibu lolote, ambapo upande wa Jamhuri ukiwashtaki kwa  makosa mawili ikiwa ni pamoja na kosa la kula njama ya kutaka kuua  na kujaribu kuua.
Miongoni mwa washtakiwa hao yupo Mume wa Albino huyo Gabriel Yohana, shemeji yake Gaudensi Yohana, Mganga wa jadi Kaponda Muyamba, Mtuhumiwa wa kutengeneza mchoro huo Linus Silukala na Mtuhumiwa aliyetaka kuununua mkono huo Mtogwa Cosmas alimaarufu kama mzee wa Ishu mkazi wa Sokomatola jijini Mbeya.
Hatahivyo mahakama hiyo iliyokuwa chini ya Hakimu mkazi Mh. Rosalia Mugisa imeweka wazi dhamana kwa watuhumiwa hao wote kwa pamoja huku mahakama hiyo ikitoa masharti manne ya dhamana hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwa na wadhamini watatu wakazi wa wilayani Sumbawanga, fedha taslimu shilingi milioni tatu kila mmoja, na mmoja wa wadhamini awe ni mwajiriwa wa serikali au Shirika lolote la umma, ambapo washtakiwa hao walishindwa maaelekezo ya dhamana hiyo na kurudishwa mahabusu hadi Machi sita itakapotajwa tena.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company