Hatufanyi kampeni Papa achaguliwe kutoka Afrika

Hatufanyi kampeni Papa achaguliwe kutoka Afrika'

Papa Benedict XVI,
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu, amesema hakuna kampeni yoyote inayofanywa na viongozi wa kanisa hilo kutoka nchi za Afrika ili kiongozi atakayechaguliwa kushika nafasi ya Baba Mtakatifu atoke Afrika.
 
Alisema hayo alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliotaka kujua kama kuna uwezekano au mpango wa nafasi hiyo kushikwa na kiongozi mmojawapo kutoka Afrika, hususan Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo.
 
“Hatufanyi kampeni yoyote kwamba, Baba Mtakatifu atoke Afrika, hususan Tanzania…hatufikirii hata mara moja kwa kigezo kwamba, atoke Afrika,” alisema Askofu Lebulu.
Alisema kanisa hilo lina mifumo ya uchaguzi, ambayo ni tofauti na inayofanyika maeneo mengine.
 
Askofu Lebulu alisema mifumo yao ni ya kiroho na inayozingatia miongozo ya kanisa, kama vile sala na kwamba, makardinali ndio wanaomchagua Baba Mtakatifu.
 
Alisema kutokana na mifumo hiyo, hakuna anayepigania au kufanya kampeni ili achaguliwe kuwa Baba Mtakatifu au kwa nafasi nyingine yoyote ya uongozi katika kanisa hilo.
 
Askofu Mkuu Lebulu alisema hayo kufuatia uamuzi wa Papa Benedict XVI, Februari 11, mwaka huu, kutangaza kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu baada ya kuliongoza kanisa hilo kwa miaka minane. 
 
Alitangaza uamuzi huo kwa hoja kuwa umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba, hawezi kuendelea kuhudumu zaidi ya umri huo.
 
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company