Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki-moon
Na
Flora Martin MwanoKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki-moon amefanya mkutano wake wa kwanza na kiongozi mkuu wa baraza la upinzani la Syria Ahmad Jarba, mkutano huo ulikuwa na lengo la kuhimiza ushiriki wao katika mazungumzo ya amani yanayolenga kutafuta suluhu ya mgogoso wa Syria uliodumu kwa takribani miaka miwili na nusu.
www.hakileo.blogspot.comKwa mujibu wa Msemaji wa UN, Martin Nesirky tayari Jarba amemuhakikishia Ban kuwa upinzani upo tayari kupeleka mwakilishi katika mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika kati kati ya mwezi Novemba.
Ban ameendelea kusisitiza umuhimu wa majadiliano ya kusaka amani na ameliomba baraza la upinzani kuyafikia makundi mengine ili wakubaliane juu ya uwakilishi wao katika mazungumzo hayo.
Makubaliano hayo yanakuja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC kupitisha azimio la kuteketeza silaha za kemikali za Syria, azimio ambalo limekuja wakati tayari wachunguzi wa silaha za kemikali za Umoja wa Mataifa wamethibitisha sumu aina ya sarini ilitumika katika shambulizi la Agosti 21 katika kitongoji kimoja mjini Damascus.
Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani yamekuwa yakiishutumu serikali ya Syria kuhusika na shambulizi hilo, tuhuma ambazo zinapingwa na serikali ya Damascus na Urusi ambao wanasema ripoti ya uchunguzi haikutaja upande uliohusika na matumizi ya silaha hizo.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Matataifa, watu zaidi ya laki moja wamepoteza toka kuanza kwa machafuko ya Syria yaliyozukwa mwezi machi mwaka 2011.