Jeshi la Nigeria, linasema kuwa
limewaua wapiganaji 150 wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko
Haram wakati wa msako dhidi yao wiki jana.www.hakileo.blogspot.com
Makabiliano yalitokea wakati jeshi lilipokuwa
linafanya msako dhidi ya wapiganaji hao katika jimbo la Borno Kaskazini
Mashariki mwa nchi.Wanajeshi wengine wa serikali wanasemekana kutojulikana waliko. Aidha jeshi lilisema pia liliweza kumuua kamanda wa wapiganaji hao Abba Goroma.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa, jeshi kwa kawaida huongeza chumvi idadi ya wapiganaji waliouawa kwa lengo la kuonyesha kuwa wanajeshi waliouawa kwenye mapigano walikuwa wachache.
Boko Haram ilianza harakati zake mwaka 2009 katika jimbo la Borno ambalo hadi sasa liko chini ya sheria ya hali ya hatari.