Serikali ya Ufaransa inasema kuwa raia wake mmoja amefariki akiwa amezuiliwa na polisi mjini Cairo.
Duru za usalama nchini humo zimesema kuwa mtu
huyo alichapwa na watu aliokuwa amezuiliwa nao hadi kufariki katika
kituo kimoja cha polisi.Mtu huyo inaarifiwa alikamatwa baada ya kukiuka agizo la kutotoka nje usiku kucha.
Agizo hilo limewekwa kama sehemu ya sheria ya hali ya hatari, iliyowekwa na serikali ya kijeshi kutokana na mgogoro uliozuka baada ya Mohammed Morsi kuondolewa mamlakani na jeshi.
Ubalozi wa Ufaransa unasema kuwa unatafuta taarifa zaidi kuhusu tukio hilo na hasa kilichosababisha kifo cha raia huyo wa raia wake ambaye alikuwa ameishi Misri kwa muda mrefu.