Mapigano yaendelea Zamboanga, Ufilipino

HABARI ZETU
Wanajeshi wakivizia wapiganaji wa MNL Zamboanga, Ufilipino
Wanajeshi wakivizia wapiganaji wa MNL Zamboanga, UfilipinoJeshi la Ufilipino linasema limewazunguka wapiganaji wanaodhibiti mji wa Zamboanga, kusini mwa nchi, baada ya siku sita za mapigano ambayo yamepelekea watu zaidi ya laki saba kuhama makwao.
Mwandishi wa BBC Barani Asia anasema risasi zimekuwa zikifyatuliwa wakati wote huku jeshi likijongelea maeneo mawili ya mwisho yenye mapigano mjini Zamboanga.
Takriban watu 65,000 inajulikana wameuwawa.

Jeshi limeripoti kuwa wengi waliouwawa ni wapiganaji wa kundi la Moro National Liberation Front, MNLF.
Raisi Benigno Aquino na makamu wake wamezuru eneo hilo Jumamosi ili kufanya majadiliano ya kutafuta amani, lakini kwa sasa inaarifiwa wanaongoza jeshi wakati linakabiliana na wapiganaji.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company