MASHINDANO YA UTANGAZAJI AJTC YAINGIA DOA.

HABARI ZETU

          SAMBOTO AHAHA KUOSHA JINA,ONESIMO AZOMEWA.
Na mwandishi wetu.
Hakuna kilichokamilika chini ya jua,usemi huu wakati mwingine husadifu yaliyopo ila kila udhaifu una uzito na uzani wake na kufanya kosa sii kosa bali kurudia kosa ni kosa.
Wakwanza kushoto ni Ndalike Said  Sonda waziri wa habari katika chuo cha AJTC.
Wakati waswahili wakiamini na kusadifu hayo wenzetu wazungu wapo kinyume nasi kwani husema kosa la kwanza ni kosa ila ukitenda jingine huwa kosa kubwa zaidi.
Sichelei wala kumungunya maneno kusema kuwa hali ya mabo kwa upande wa chuo cha AJTC hayaendi  kama ilivyo pangwa, nayanena hayo kutokona na mambo mbali mbali ya nayo endelea hivi sasa.
Ikumbukwe ya kwamba mashindano haya yalianza Jumatatu ya wiki hii na yanatarajia kuitimishwa rasimi ijumaa hii,Mashindano haya yana husisha madarasa yote ya chuo hiki huku madarasa ya ngazi ya cheti na stashahada ya kiwa katika makundi tofauti kwa lengo la kupata vinara wa makundi yao ili siku ya ijuma ya weze kuchuana katika hatua ya mwisho.
Katika siku ya kwanza tulishuhudia mapungufu kadhaa ikiwemo ya washiriki kuto kusikika vizuri hali iliyosababishwa na mipangilio mipaya ya vyombo vilivyo tumika.
Kama hayo hayatoshi baadhi ya washiriki akiwemo Goodwill ambae ni mshiriki kutoka katika darasa la Selou alilalamikia kitendo cha darasa la Kilimanjaro cha kuchomoa nyaya na kisha kuzima computa ikiwa ni hujuma iliyo lenga kumdhoofisha kisaikolojia na kumpotezea muda.
Goowill hakufanya
vizuri na aliangazia ya kwamba sababu kubwa ni hujuma hiyo,katika hali ya kushangaza uongozi ama majaji wanao simamamia shindano hili la utangazaji hawakuchukua hatua zozote.
Pia Goodwill hakuishia hapo bali alilamikia kitendo cha kupewa dakika 10 tu kwaajili ya kuendesha kipindi malumu muda alioita kwake ni mdogo ukizingatia ya kwamba alijianda kuendesha kipindi cha nusu saa na waandaji hawakumpa taarifa kabla.
Na hili ni japo la majaji wanao toa hukumu kwa washiriki wa shindano hili,wakwanza kutoka kushoto ni Luckas Modaha,akifwatiwa na Chao,Samboto,Verediana Akonai, na Izack aliinamisha kichwa ni Elliua Onesimo


Alievaa tisheti nyekundu ni Lasco Chua na wengineo ni wanafunzi wenzake katika chuo hiki wakifwatilia mashindano haya.
Katika hatua nyinmgine hiyo jana mashindano hayo yalilazimika kurudiwa baada ya kusadikika ya kwamba wakati madarasa ya ngazi ya cheti ya kishindanda vyombo vilikuwa havija fungwa vizuri.
Swali la kujiuliza na lisilo na majibu ni kwamba,majaji hawakuisika sauti hiyo kabla ya washiriki wote kumalizia na swali la pili ni kwa nini hawakukagua mitambo kabla ya kuruhusu washiriki kuchuana.
Swali la tatu liloonekana kuibua jaziba kutoka kwa wadau wengi lililenga kuhoji ya kwamba ni kwanini utaratibu huo usingali tumika kwa washiriki waliofungua dimba siku ya kwanza ambao wengi wao hawakusikika vizuri.
Kama hayo hayatoshi kuna baadhi ya washindi walio tangazwa hawa kukidhi vigezo ikiwemo kuto kumaliza muda na kutokuaga lakini cha ajabu walitangazwa kuwa washindi.
Pia mshindi wa kipindi malumu kwa darasa la Ould Zungwa aliingiza wageni studio pamoja na Nassoro ambae ni mshindi wa  darasa la Kilimanjaro kwa upande wa kipindi malumu pia,kwa mujibu wa mwalimu ambae pia ni jaji E. Sambo aliponda kitendo na kudai ya kwamba ni uvivu wa hali ya juu.
Doa jingine lilo msababisha Majaji kufika na kutupa shutuma kubwa kwa wahusika  ni kitendo cha baadhi ya wanafunzi ambao majina yao hayakuwekwa bayana cha kupeleka mashitaka kwa wakuu wa chuo kitendo walicho kiita cha kinafiki,majungu na  uzandi,kwangu huu ni msamiati mpya na wakigeni.
Inawezekana wanafunzi hao walifanya hivyo kwa nia na dhamira njema ila tafsiri zilizo tokana na mapokeo finyu ndio chanzo cha kugadhabika kwao.
Kwa mujibu wa majaji hao walidai ya kwamba malalamiko yote yalipaswa kupitia kwao, lakini wanasahau ya kwamba kesi ya nyanyi huwa haipelekewi kwa ngedere na ingaliwezekanaje wakati muandaji mkuu ama msimamizi mwalimu Onesimo alivyo kuwa akihojiwa studio siku ya jumatatu iliyopita alisema ya kwamba hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa.
Sasa kuna haja gani kumpelekea mtu ambae hata kusikiliza wala kuchukua hatua na ni mashindano gani ambayo hayana kamati ya rufaa ? Na kama ni mtu unaejiamini na kazi yako kwanini ulalamikie kitendo cha wao kupeleka malalamiko kwingineko?
Tuache uwoga wakuto kujiamini inawapasa kujiamini kwa kile wanacho kifanya madamu tuu wawe wamesimamia  haki na kutekeleza wajibu wao ipasavyo.Yawapasa kutambua ya kwamba kila mtu anamapokeo yake na pale waonapo mapungufu yao hawana budi kujirekebisha kwani kukiri udhaifu sio dhambi.
Kabla sija maliza ngoja ni wape kihoja cha mwaka,kwa muji wa taswira ama kanuni za mashindano kila mtu anayo haki ya kushiriki ama kuto kushiriki mashinda yoyote lakini katika AJTC mambo ni tofauti kwani darasa la Tanganyika lilipewa adhabu eti kisa na mkasa hawakuandika muongozo wa kipindi wenye kiwango sitahiki.
Ni jopo hilo hilo la majaji,wakwanza kutoka kulia ni Madam Prica akifwatiwa na Jaji Ngobole
na Izzack Chiwanga,wengine wameshatajwa kwenye picha ilio tanguliawww.hakileo.blogspot.com.
Kwa kumalizia ni peleke pole zangu kwa darasa la stashahada Serengeti kwakushindwa kusoma tarifa ya habari leo kutokona na mwenye habari hizo kuzisahau mbali ambako ni Njiro.
Ila waandaji wangalikuwa na busara wange waongezea muda kwa kuruhusu madarasa mengine kwanza na kama muda wote ungali malizika habari zikiwa bado ndipo hatua nyingine zingefwata.
Nimalizie kwa kusema ya kwamba ni haki na umakini pekee ndio unaoweza kuwafanya wanafunzi au wadau kuacha vitendo vya kunun’gunika ama kuzomea kama vilivyo mkumba mwalimu Onesomo jana na sio njia za mlango wa nyuma za kujisafisha kama alivyo kuwa akifanya mwalimu na Jaji Samboto jana kwa kushirikiana na Izack, kwa kifupi wanafunzi hawa sio vichaa wala wehu kwani hujua lipi baya na lipi jema.
                      Na mdhaifu hukwepa lawama.
Tafadhali kwa maoni au ushauri wasiliana nami; 0759859287 au barua pepe: hakileotanzania@gmail.com



Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company