Vikosi vya Kenya na wafanyakazi wa uokoaji walitafuta kwa undani katika mabaki ya maduka makubwa ya Westgate mjini Nairobi (tarehe 25 Septemba) miili na milipuko iliyotegwa baada ya
kuzingirwa kwa siku nne na al-Shabaab kwenye maduka hayo yaliyosababisha watu 67 kufariki dunia na dazeni kadhaa hawajulikani waliko.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitangaza tarehe 24 Septemba kwamba uzingirwaji wa maduka makubwa ya Westgate ya Nairobi umekwisha, lakini alisema hasara zilizotokana na shambulio lililofanywa na al-Shabaab zilikuwa "kubwa sana" na watu wapatao 67 walifariki dunia. Alitangaza siku tatu za maombolezo ya taifa. [AFP]Play VideoWatu wakiangalia orodha ya
www.hakileo.blogspot.comwaathirika wa shambulio la maduka ya matajiri ya Westgate nje ya hospitali ya M P Shah huko Nairobi tarehe 24 Septemba, 2013. [Simon Maina/AFP]
Waokoaji walivaa mabarakoa na baadhi ya maaskari walivaa skafu kuzunguka midomo yao kwa sababu ya harufu mbaya ndani ya jengo hilo. Sehemu kubwa ya jengo ilibomoka baada ya milipuko mikubwa na upigaji wa risasi za silaha nzito.
Nchini kote Kenya, bendera zinapepea nusu mlingoti kuanza siku tatu za maombolezo rasmi.
Pamoja na hayo yote
al-Shabaab ilidai kuhusika na uzingiraji huo lakini siku ya Jumatano wanamgambo hao walio shirika na al-Qaeda walilaumu serikali ya Kenya kwa kutumia kemikali ili kumaliza hali hiyo, kuua mateka 137 katika mchakato huo.
Idadi ya al-Shabaab haiwezi kuthibitishwa na ni kubwa kuliko idadi ya watu walioandikishwa rasmi ambao hawajulikani waliko.
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya Kanali Cyrus Oguna na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mutea Iringo walikataa kutoa maoni kuhusu madai ya al-Shabaab kwamba vikosi vya usalama vilitumia kemikali.
Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), makao Makuu ya Idara ya Upelelezi wa Jinai ya Uingereza na wana usalama wa Israeli wanaisaidia Kenya kutafuta ushahidi unaohitajika na mahakama, Iringo aliiambia Sabahi.
Jeshi la Kenya pia lilipokea ushauri kuhusu mbinu na operesheni za kiutaalamu, alisema.
Kadri uchunguzi unavyoendelea, maswali mengi yanabakia juu ya utambulisho wa washambuliaji, uwezekano wa kuhusika kwa mwanamke wa Uingereza anayeaminika kuwa ni
'Mjane Mweupe' Samantha Lewthwaite na wanajihadi wengine wa nje, na namna kikundi hicho kilivyoingiza silaha nyingi na risasi katika jengo.