Spika wa baraza la wawakilishi John Boehner, R-Ohio, akielekea kwenye Baraza la wawakilishi kupiga kura yake kwenye bunge la Marekani Washington,
Rais Barack Obama amelihutubia taifa Jumatatu usiku akisiistiza kwamba jeshi la taifa litaendelea na kazi zake wakati sehemu za serikali kuu zinafungwa kuanzia Jumanne baada ya bunge kushindwa kukubaliana juu ya bajeti ya mwaka 2013 - 2014.
www.hakileo.blogspot.com
Baada ya wabunge wa Baraza la Wawakilishi kushindwa kukubaliana ilipofika usiku wa manane Jumatau, juu ya bajeti ya matumizi, serikali kuu ililazimika kutangaza kwamba sehemu za idara kadha zitabidi kufungwa.
Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea bungeni kuhusiana na sheria ya kihistoria ya Rais Obama, ya kutowa huduma nafu za afya ambayo imekuwa mashuhuri kwa jina la "Obamacare".
Baraza la wawakilishi linaoongozwa na Warepublican liliidhinisha mswada wa matumizi ya serikali lakini kwa kuambatanisha kufutwa kwa sheria ya Obamacare. Na mara tatu Baraza la Senet linalodhibitiwa na wademokrat limepinga mswada huo.
Kutokanana Bunge kutokubaliana juu ya kupitisha mswada wa kuongeza muda wa matumizi ya serikali kuu sheria ya Marekani inahitaji idara zote ambazo hazina shughuli muhimu kusita kufanya kazi kuanzia Oktoba mosi, yani siku ya Jumanne.