Obama amesema shambulizi la Marekani huko Syria litakuwa lenye malengo maalum katika kuharibu matumizi ya kemikali.
Rais amesema hatapeleka wanajeshi wa Marekani huko Syria na hatafanya operesheni isiyojulikana mwisho wake kama vile Iraq na Afghanistan na mashambulizi ya ndege ya muda mrefu kama ilivyokuwa Libya au Kossovo.
Amesema anajua hali mbaya ya vifo viliyosababishwa na vita vya Iraq na Afghanistan , kwamba wazo lolote la vita halitapendwa na watu.