UN yajadili azimio kuhusu Syria


Serikali ya Syri ainadaiwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake na kusababisha maafa makubwa
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linajadili rasimu ya azimio kuhusu silaha za kemikali za Syria baada ya Marekani na Urusi kukubali mapendekezo ya azimio hilo.
Wanachama kumi na tano wa baraza hilo huenda wakapigia kura azimio hilo baadaye leo, hii ni kwa mujibu wa wanadiplomasia katika umoja wa Mataifa.

Inaonekana kama hatua muhimu katika mwafaka unaosakwa sana kwa ushirikiano wa Marekani na Urusi ambapo Syria itafichua zana zake za kemikali na kuziharibu ifikapo
mwaka 2014Makubaliano hayo yanamaliza mvutano wa miaka miwili na nusu katika www.hakileo.blogspot.comUmoja wa mataifa kuhusu Syria.
Urusi na China mara tatu zimekuwa zikizuia maazimio ya nchi za magharibi katika baraza la usalama dhidi ya Rais wa Syria, Bashar al-Assad.
Baraza hilo lilijadili azimio hilo Alhamisi Jioni katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Kabla ya mkutano huo Marekani na Urusi zilitofautiana kuhusu maandiko na mapendekezo ya azimio hilo.
Marekani kwa ushirikiano na Ufaransa na Uingereza, zilikuwa zimependekeza kuchukau hatau za kijeshi dhidi ya Syria.
Urusi nayo ilipinga azimio hilo kwa sababu ya tisho la kuvamia Syria kijeshi.
Mataifa hayo ni wanachama wenye uwezo wa kupiga kura ya turufu dhidi ya pendekezo lolote katika baraza hilo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company