Bunge la Tanzania
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Tanzania wamesisitiza madai yao ya kutaka kurejeshwa bungeni muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ili kuendelea na mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya yenye ridhaa ya watanzania wote.
Wakizungumza katika mahojiano maalum na sauti ya Amerika-VOA viongozi hao Freeman Mbowe wa CHADEMA, James Mbatia wa NCCR MAGEUZI na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF wamesema kilichofanyika bungeni kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi-CCM kupitisha muswada huo wa sheria ya mabadiliko ya katiba kibabe kutaliweka taifa katika wakati mgumu kupata katiba bora yenye maslahi kwa watanzania wote
.