Polisi wa Afrika Kusini wanatuhumiwa kwa kudanganya kuhusu mauaji ya Marikana yaliyotokea mwaka jana, ambapo wachimba migodi 34 waliuawa. Taarifa hii ni kwa mujibu wa tume ya uchunguzi iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza mauaji hayo.
Inasemekana polisi walitoa ushahidi wa uongo au kuficha nyaraka ambazo zilitoa taarifa za uongo kuhusu matukio katika mgodi huo.
Polisi walisema kuwa walikuwa wanajikinga kutokana na kuvamiwa na wachimba migodi hao siku chache baada waandamanaji kudaiwa kuwanyonga polisi wawili.Kitendo cha polisi kuwauawa kwa kuwapiga risasi wachimba migodi katika mgodi unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin kiliwashtua sana wengi nchini humo.www.hakileo.blogspot.com
Tume ihiyo iliteuliwa na Rais Jacob Zuma kuchungza mauaji hayo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuwahi kufanywa na polisi tangu kukamilika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi.
Taarifa yake ambayo imekuja siku kumi baada ya kupata taarifa za polisi kwenye komputa zao na pia kupitia nyaraka zao.