WAZIRI CHIKAWE, KATIBA NA KELELE ZA WAPINZANI....!

islammboye_be136.jpg
Ndugu zangu,
Imeripotiwa kwenye gazeti la Mwananchi, leo Ijumaa Septemba 20,kuwa Waziri wa Sheria na Katiba, Mheshimiwa Chikawe, amemwomba Rais Kikwete asaini Muswaada wa Marekebisho ya sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa na Bunge Septemba 6, mwaka huu. Kwamba Rais afanye hivyo ili kuepuka vurugu.
www.hakileo.blogspot.com
Hakika, huu ni wakati wa kuongozwa zaidi na hekima na busara kuliko hisia na ushabiki na hususan wenye sura za vyama na kuangalia maslahi ya muda mfupi na ya kibinafsi zaidi.(P.T)
Rais wa Nchi anaongoza watu, na si mawe. Msingi wa kukubalika kisiasa ni lazima utokane na kukubalika na watu. Na wapinzani hao pia nyuma yao si mawe yaliyojipanga. Ni watu. Hivyo basi, inahusu watu. Inahusu Wananchi. Katiba ni mkataba baina ya watu katika jamii. Si miti na mawe.
Hivyo, ni muhimu sana watu kwa maana ya wananchi wakasikilizwa. Kama kuna manung'uniko yatafutiwe majawabu ili tufike salama kwenye kulifikia lengo kuu; Katiba ya Wananchi. Si ya chama tawala wala vyama vya upinzani. Ni jambo litakalotupeleka hata miaka 100 ijayo.
Maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana. Wengi wetu hatutakuwepo, hata pale nchi yetu itakapotimiza miaka 100 ya Uhuru. Desemba 9, 2061.
Na Waziri Chikawe asiwe na hofu. Watanzania kwa desturi si wapenda vurugu. Hata katika hili la Katiba hawatafanya vurugu. Ila wakipewa nafasi ya kuonyesha masikitiko yao, basi, watayaonyesha, bila kufanya vurugu.
Maggid.
Iringa.
0754 678 252
Comments!
Nelson Msita Mie huwa najiuliza hivi hawa mawaziri wa chama tawala..huwa wanajiongoza kwa akili zao au kwa akili za chama.!?na kama ni kwa akilo za chama je chama kimetoa wapi akili hizo..:?
22 minutes ago via mobile · Like

Mtanzania Kihange Ni vyema Busara ikitumika na sio mitazamo ya watu binafsi

20 minutes ago via mobile · Like

Muhidin Thabeet Kiss Bado Naendelea Kuamini Matatizo Mengi Yanayoikumba Nchi Yetu Yanatokana na Kukosa Busara na Hekma Kwa Viongozi Wetu.

19 minutes ago · Like

Rashid Katakwa ni vizuri tukakumbuka ya kwamba ktk serikali ya rais jk,hakuna hata kiongozi mmoja aliyekuwa na wazo la katiba hata chama chake hakikuwa na ajenda ya katiba,ni busara za rais jk za kuazisha mchakato wa katiba,kwa busara hizo hizo naamini atatuvusha salama hao kina chikawe na wenzake hawajui watendalo!

10 minutes ago · Edited · Like

Mtumishi Stanley Mngoni Rashid unasema ni busara za JK kuanzisha mchakato wa katiba una uhakika na kauli yako?

8 minutes ago · Like

Rashid Katakwa ndio!kwani ilikuwa ktk ilani ya chama chake?

7 minutes ago · Like

Rashid Katakwa katiba haikuwa ktk ilani ya ccm!karibia vyama vyote vya upinzani walitaka katiba mpya!shinikizo toka kwa vyama pamoja na asasi za kiraia kupiga kelele ndio maana jk akatumia busara kusikiliza kelele za wengi!ni busara tu ndugu yangu au ww busara unaitafsiri vp?@mngoni
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company