130 wafa maji wakijaribu kwenda Ulaya



Wahamiaji wakiokolewa kutoka baharini

Maafisa katika kisiwa kikubwa cha Sicily katika bahari ya Meditarenia wanasema kuwa wamepata maiti 130 baada ya mashua iliyokuwa imewabeba takriban wahamiaji 500 wa kiafrika kushika moto na kuzama katika kisiwa cha Lampedusa.

Boti hiyo ilikuwa safarini kuelekea Ulaya lakini ikazama katika kisiwa cha Lampedusa katika pwani ya Utaliana
Inaarifiwa abiria walijirusha baharini wakati moto ulipozuka ndani ya botiTakriban miili 103 imepatikana baharini na mingine zaidi kupatikana ndani ya boti iliyozama.

Zaidi ya wahamiaji 150 wameokolewa.

Wengi wa wahamiaji hao walikuwa raia wa Eritrea na Somalia,kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Shughuli kubwa ya uokozi ingali inaendelea kuwatafuta manusura kwani inahofiwa mamia zaidi huenda wamefariki kutokana na ajali hiyo.

Meya wa mji huo anasema kuwa walionusurika wako hatika hali ya mshutuko na walimwambia kuwa moto mdogo uliwashwa baada ya meli kukwama na lengo lilikuwa kuitisha msaada.

Lakini alisema kuwa moto ulisambaa kupita kiasi na ikawa vigumu kuudhibiti.

Kisiwa cha Lampedusa kiko kati ya Tunisia na Sicily na kimekuwa kiingilio kikuu cha wahamiaji kuingia barani Ulaya.www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company