Waziri wa Mambo ya ndani wa Ufaransa Manuel Valls
Serikali ya Ufaransa na ile ya Mexico zimetaka maelezo ya kina toka kwa utawala wa Marekani kuhusu tuhuma kwamba nchi hiyo imekuwa ikirekodi mawasiliano ya simu kwa mamilioni ya raia wake.
Ufaransa kupitia kwa waziri wake wa mambo ya kigeni, Laurent Fabius imemuandikia barua balozi wa Marekani nchini humo ikimtaka atoe maelezo kuhusu tuhuma zinazoikabili nchi ya Marekani.
Marekani inatuhumiwa kufanya ujasusi kwenye mawasilianao ya raia wa Ufaransa kufuatia taarifa za siri zilizovujishwa na jasusi wazamani wa Marekani, Edward Snowden.
Manuel Valls ni waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, anasema kitendo kilichofanywa na Marekani hakikubaliki.
Kauli hiyo ya Ufaransa inatolewa wakati huu ambapo waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amewasili nchini humo kwa mazungumzo na wakuu wa Ufaransa kuhusu mzozo wa Syria pamoja na uhusiano wa mataifa hayo mawili.