Wanajeshi wa serikali ya Congo FARDC wamethibitisha mapigano kuendelea Mashariki mwa DR Congo
REUTERS/Thomas Mukoya
Na
Martha Saranga AminiMapigano yameendelea kushuhudiwa kati ya waasi wa m23 dhidi ya jeshi la serikali ya Jamuhuri ya demokrasia ya Congo huko mashariki mwa nchi hiyo wakati huu jumuiya za kimataifa zikitoa wito wa kukomesha mapigano na kurejea katika mazungumzo ya amani.
Kwa mujibu wa jeshi la DR Congo Mapigano yameshuhudiwa Kibumba, takribani kilometa 25 kaskazini mwa Goma,eneo lenye utajiri wa madini.
Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu kutoka eneo la kibumba amesema milipuko imeendelea kusikika usiku kucha.
Hata hivyo Bertrand Bisimwa, kiongozi wa kundi la waasi wa M23 Ambalo limepiga kambi jirani na mpaka wa Rwanda amesema jeshi la serikali limeanzisha mashambulizi dhidi ya waasi eneo la mabenga karibu kilomita 90 kaskazini mwa Goma.
Mapigano ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yaliripotiwa kuanza siku ya Ijumaa, siku chache baada ya mazungumzo baina ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23 kukwama.
ujumbe wa kulinda amani kutoka Umoja wa Mataifa MONUSCO,umesema ijumaa kuwa umeguswa sana na ukatili na uadui unaoibuka upya na kutoa wito kwa waasi wa M23 kurudi katika meza ya mazungumzo.