Jarida la habari la Ujerumani la Der Spiegel, limeripoti kuwa mashirika ya ujasusi ya Marekani yamekuwa yakichunguza simu ya mkononi ya Kansela Angela Merkel tangu mwaka 2002. Jarida hilo limeripoti jana Jumamosi kuwa rais Barack Obama alimuambia Kansela huyo wa Ujerumani kuwa angesitisha udukuzi huo kama angelijua kuwa unafanyika.
Ufichuaji wa taarifa za kudukuliwa kwa mawasailiano ya simu ya mkononi ya Merkel na idara ya usalama wa taifa ya Marekani NSA, umesababisha hasira nchini Ujerumani, na kuilaazimu serikali kumuita balozi wa Marekani kutoa maelezo. Der Spiegel lilisema idara maalumu ya kukusanya taarifa ilikuwa ikitumia vifaa vya kisasa zaidi kuichunguza serikali ya Ujerumani kutokea ubalozi wa Marekani mjini Berlin.
Kwa kutumia waraka wa siri wa mwaka 2010, jarida hilo liliongeza kuwa NSA ilikuwa inaendesha vituo vingine 80 sawa vya ujasusi duniani kote. Serikali imesema kuwa maafisa wa idara ya ujasusi ya Ujerumani watasafiri kwenda mjini Washington kukutana na wenzao katika wiki zijazo ili kupata maelezo.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago