ECOWAS kuanzisha mfumo mmoja wa ushuru





Nchi wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS zimekubaliana kuwa na mfumo wa pamoja wa ushuru wa forodha ifikapo mwaka 2015 ikiwa ni katika jitihada za kuharakisha utangamano wa kiuchumi katika kanda hiyo. Mkuu wa kamisheni ya ECOWAS Kadre Desire Ouedraogo, amesema, hilo ni lengo ambalo limekuwa likipiganiwa kufikiwa na jumuiya hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 38 iliyopita. Makubaliano hayo yaliyofikiwa na wakuu wa nchi 15 wanachama wa ECOWAS yanalenga kuwa na kima kimoja cha ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa ndani ya nchi hizo zenye idadi ya watu wapatao milioni 300. Hivi sasa tayari nchi nane kati ya 15 wanachama wa ECOWAS zina mfumo wa pamoja wa ushuru wa forodha na sarafu ya pamoja. Nchi hizo zinazounda Umoja wa Uchumi na Fedha wa Magharibi mwa Afrika UEMOA ni Benin, Burkina Faso, Ivory Coast, Guinea, Guinea-Bissau, Senegal, Niger na Togo. Jumuiya ya ECOWAS imepanga kuanzisha sarafu ya pamoja kwa nchi zote wanachama ifikapo mwaka 2020. Kwa mujibu wa Mkuu wa Kamisheni ya ECOWAS uamuzi wa kuanzisha mfumo mmoja wa ushuru wa forodha utawezesha kuanzishwa tena mazungumzo yaliyokuwa yamekwama kati ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo na Umoja wa Ulaya EU ya Makubaliano ya Ushirika wa Kiuchumi (EPA). Umoja wa Ulaya ndiye mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi za Magharibi mwa Afrika…/
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company