

Habari za kusikitisha ambazo tumezipata kutoka mkoani morogoro asubuhi hii ni kuwa mtangazaji mkongwe hapa nchini Julius Nyaisanga maarufu kama "Uncle J" amefariki dunia
Hadi Julius Nyaisanga anafariki dunia alikuwa meneja wa kituo cha redio Abood FM cha mjini Morogoro, na alijulikana sana tangu akifanya kazi Redio Tanzania sasa hivi inajulikana kama TBC Taifa na Redio One stereo.