Wafuasi wa Muslim Brotherhood wakiandamana kupinga kuondolewa kwa Rais Mohammad Morsi
Vyombo vya habari vya Misri vinaripoti kuwa serikali ya nchi hiyo imemtia mbaroni mwanasiasa maarufu Essam El Arian ambaye pia alikuwa ni mwanachama wa Muslim Brotherhood na Makamu Mwenyekiti wa chama chaJustice and Freedom.
Bwana El Arian ametiwa mbaroni katika mji mkuu wa Kairo.
Hapo awali mwendesha mashtaka wa nchi hiyo aliagiza Essam El Arian akamatwe tangu mwezi July baada ya Rais Mohammad Morsi ambaye pia alikuwa ni mwanachama wa Justice and Freedom kuondolewa madarakani.