Rais Obama asema yuko tayari kuzungumza na wabunge wa Republican kuhusu Bajeti


Rais wa Marekani Barrack Obama
Rais wa Marekani Barrack Obama anasema yuko tayari kuzungumza na wabunge wa Republican kuhusu kupitishwa kwa bajeti muhimu ili kurejesha huduma za serikali zilizokwama wiki iliyopita, na kuwataka kuacha vitisho vya kutikisa uchumi wa taifa hilo ili kuweka doa katika uongozi wake.

Obama amewaambia wanasiasa wa Republican kuwa ni kama watu ambao wanataka kikombozi ili kufanya kazi yao.

Wiki iliyopita, maelfu ya wafanyikazi wa Serikali nchini humo walirudi nyumbani baada ya kukosa kazi kwa kutokuwepo kwa fedha za kufanikisha huduma muhimu za serikai baada ya wabunge wa Republican kukataa kupitisha bajeti hiyo muhimu.

Wabunge wa Republican wakiongozwa na Spika wa Congress John Boehner qwamesema kuwa wao wako tayari kwa mazungumzo lakini wanasikitishwa na hatua ya rais Obama kukataa kuzungumza nao.

Boehner ameongeza kuwa hatua ya rais Obama kuwataka wao kujisalimisha na kukubali sera zake ni hatari sana kwa uchumi wa Marekani ambao huenda ukadorora ikiwa suluhu halitapatikana kufikia tarehe 17 mwezi huu kwa sababu serikali itafikia mwisho wa kukopa fedha.

Rais Obama kwa upande wake amemjibu Spika Boehner kwa kumwambia kuwa ana uwezo wa kufungua huduma za serikali kwa kuruhusu wabunge wa Congress kupiga kura kuamua ikiwa wanataka huduma za serikali zirejelewe au la.

Wabunge wa Republican wanasema kuwa walichukua hatua hiyo, ili kuchelewesha sera ya raia Obama kuhusu bima ya afya, mpango ambao rais Obama ameendelea kusisitiza kuwa hautabadilishwa.www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company