Raisi wa jamuhuri ya demokrasia ya Congo,DRC Joseph Kabila RFI


Raisi wa jamuhuri ya demokrasia ya Congo,DRC Joseph Kabila

Raisi wa jamuhuri ya demokrasia ya Congo DRC Joseph Kabila amesema serikali ya muungano wa kitaifa itaundwa katika siku za hivi karibuni ikijumuisha makundi mbalimbali kutoka ndani ya taifa hilo.

Akizungumza katika hotuba yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu raisi Kabila amesema serikali ya muungano itaundwa na wanasiasa kutoka vyama vinavyomuunga mkono na vya upinzani wakiwemo wawakilishi wa mashirika ya kiraia.

Raisi Kabila amebainisha majukumu ya Serikali ya kiraia itakayoundwa nchini Jamuhuri ya demokrasia ya Congo itakuwa ni kurejesha amani na utawala bora wa serikali katika nchi nzima,kuimarisha mshikamano wa kitaifa pamoja na kufuatilia sera ya utawala wa majimbo lakini pia kushughulikia maandalizi ya uchaguzi na kuboresha maisha ya raia.

Hotuba hii imetolewa hii leo Jumatano huku wananchi wa mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakiwa na mashaaka kuhusu utekelezwaji wa azma ya serikali ya Kinshasa kulishughulikia suala la mapigano yanayojiri katika eneo hilo.

Wachambuzi wa masuala ya Kijamii wanasema Hawana imani kuona mazungumzo yaliyokuwa yanafanyika mjini Kampala Nchini uganda baina ya wajumbe wa serikali ya Congo na waasi wa kundi la M23 yanaokoa Hali ya mambo katika Eneo Hilo, licha ya wito wa jumuia ya kimataifa kwa pande zinazohusika kuhakikisha Mazungumzo hayo yanatamatika baada ya Kuupata Ufumbuzi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company