NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe juzi alilazimika kuhutubia mkutano wa hadhara wilayani Kaliua, Tabora kwa njia ya simu akiwa jijini Dar es Salaam ili kuwanusuru viongozi wa chama hicho.
Viongozi walionusurika kupigwa ni Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa CHADEMA, Msafiri Mtemelwa, wenyeviti wa chama wa mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma na mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi.
Dalili ya viongozi hao kuwa katika wakati mgumu zilianza kuonekana mapema wakati msafara wao ulipofika katika Kijiji cha Ibambo, Kata ya Mwongozo bila Zitto kuwepo.
Matangazo ya awali ya mkutano wa CHADEMA yalisema kuwa Zitto angekuwepo, lakini kiongozi huyo alisitisha ziara yake ya kuimarisha chama ili kurejea Dar es Salaam kuhudhuria kamati za Bunge.
Katika Kijiji cha Mwendakulima, umati wa wananchi uliridhika baada ya viongozi kuwahakikishia kuwa Zitto atakuwepo katika mkutano wa mwisho uliofanyika Uwanja wa Mnadani wilayani Kaliua.
Hata hivyo, kabla ya msafara wa viongozi kufika uwanjani hapo, baadhi ya waandishi wa habari waliwasiliana na Zitto kumuelezea hatari inayowakabili wenzake baada kutoonekana.
Zitto alisema kuwa alikosa ndege na kuahidi kurejea katika Wilaya ya Kaliua kabla ya kufanya ziara katika Mkoa wa Kigoma.
Baada ya wananchi kubaini kutokuwepo kwa Zitto, walizuia gari la matangazo lisiondoke na kumtaka Mtemelwa ampigie simu ili wasikie kauli yake, vinginevyo msafara wao usingetoka salama uwanjani hapo.
Kutokana na hali hiyo, Mtemelwa alimpigia simu Zitto na kisha kuunganisha mazungumzo yao katika kipaza sauti uwanjani hapo.
Zitto aliwaomba radhi wananchi wa Kaliua kwa hali iliyojitokeza na kuwaahidi kuungana nao wakati mwingine.
“Naomba muendelee na moyo huo huo kwa ajili ya CHADEMA, niliahidi kuwa nanyi leo ila nimeshindwa kwa sababu ya kukosa usafiri wa kunifikisha huko, wasikilizeni viongozi mlionao nami nitaungana nanyi wakati mwingine, nawaomba msamaha kwa hali ilyojitokeza,” alisema.
Katika hotuba yake kwa njia ya simu, Zitto aliwaeleza wananchi juu ya umuhimu wa kujua haki zao za msingi na namna Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinavyowasahau wakulima na kuwakumbatia wawekezaji huku nchi ikiendelea kubaki katika umasikini.
Wananchi waliozungumza na gazeti hili uwanjani hapo, walimuahidi Zitto kuwa wanaruhusu msafara uendelee katika maeneo mengine kwa sharti la yeye kurudi katika eneo hilo, vinginevyo waachane na CHADEMA.
“Tumeahirisha mkutano mara tatu, kila siku tunaambiwa Zitto amepata dharura, ndiyo maana leo tulitaka kuwashughulikia hawa viongozi waliokuja bila Zitto,” alisema mmoja wao.
Awali katika Kijiji cha Mwendakulima, wananchi walieleza namna chama cha msingi kinavyowadhulumu fedha za mauzo ya tumbaku na kwamba wanaohoji juu ya hilo hufukuzwa uanachama.
Walisema tayari wanachama zaidi ya 180 wameshafukuzwa kutokana na kudai fedha za mauzo ya tumbaku.
Katika Kijiji cha Ibambo, Kata ya Mwongozo, CCM ililalamikiwa kupora jengo la wananchi na kulifanya mali yake.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ibambo, Erasto Mazinge aliwaeleza hayo baada ya waandishi kutaka ufafanuzi wa ofisi ya serikali kuwa katika sehemu moja na ofisi za CCM.
Mazinge alisema licha ya wananchi kujenga jengo la vyumba nane kwa matumizi ya serikali, CCM iliamua kuwabadilikia na kulifanya ni jengo la chama.
Kauli ya Mazinge inaungwa mkono na John Kapongo, Katibu wa Tawi la CCM Mwongozo, aliyesema chama chake kilitumia mbinu ya kuwalaghai wananchi kujitolea kujenga jengo hilo kwa ajili ya matumizi ya serikaliawww.hakileo.blogspot.com
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago