Tuzo ya Mo Ibrahim yakosa mshindi kwa mara ya tatu


Dr.Salim Ahmed Salim mmojawapo wa Viongozi waliopo katika jopo la Kuchagua mshindi wa tuzo ya Mo Ibrahim
Na Martha Saranga Amini

Kwa mara ya tatu mfululizo katika kipindi cha miaka mitano tuzo maalumu kwa viongozi wa Afrika inayotolewa na taasisi wa Mo Ibrahim imeshindwa kutolewa kutokana na kukosekana kwa kiongozi ambaye anastahili kupokea tuzo hiyo.



Kukosekana kwa mshindi kwa mwaka wa tatu mfululizo kunazua maswali kuhusu vigezo vinavyotumiwa na taasisi hiyo kupata mshindi huku baadhi wakishauri kubadilishwa kwa vigezo vyake jambo ambalo linapingwa vikali na Dr, Salim Ahmed Salim mmoja wa jopo linalotazama vigezo hivyo.

Kwa upande wake Mo Ibrahim yeye hajutii kukosekana mshindi kwa mwaka wa tatu mfululizo badala yake anaona hii ni changamoto kwa viongozi wa Afrika kutekeleza majukumu yao kwa wananchi na kukabiliana na vitendo vya rushwa huku pia akisisitiza kutobadilishwa kwa vigezo vya kupata mshindi.

Viongozi wa nchi waliowahi kuibuka washindi na kutunukiwa tuzo hiyo ni Joaquim Chissano wa Msumbiji, Rais Festus Mogae wa Botswana mwaka 2008,huku Mara ya mwisho tuzo hii ikitolewa mwaka 2011 kwa rais wa Cape Verde wakati huo, Pedro Pires.

Hata hivyo, Tuzo ya Mo Ibrahim haikutolewa mwaka 2009 na 2010 kutokana na kilichoelezwa na Kamati ya tuzo hiyo kuwa ni kukosekana kwa washindi marais waliotimiza vigezo vya utawala bora barani Afrika jambo ambalo safari hii linazua maswali mengi barani Afrika na kwingineko.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company