Wanafunzi wa kidato cha pili kufanya mtihani



Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
Na Raymond Kaminyoge
                             KWA UFUPI
Alisema watahiniwa waliojiandikisha wanajumuisha makundi maalum yenye uoni hafifu, ambao ni 89 na wasioona 93.
Dar es Salaam. Jumla ya watahiniwa 531,457 wa kidato cha pili wanatarajia kufanya mtihani utakaoanza kesho Oktoba 7 hadi 21 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema mitihani hiyo itafanyika kwa wiki mbili.
Alisema kati ya idadi hiyo, wasichana ni 270,734 sawa na asilimia 50.9 na wavulana ni 260,723 sawa na asilimia 49.1.
Mchome alisema katika taarifa yake kwamba idadi ya shule na vituo vilivyosajiliwa kufanyia mtihani huo mwaka huu ni 4,437 ikiwa ni ongezeko la vituo 140 sawa na asilimia 3.3 ikilinganishwa na vituo 4,297 vilivyosajiliwa mwaka 2012.
Alisema watahiniwa waliojiandikisha wanajumuisha makundi maalum yenye uoni hafifu, ambao ni 89 na wasioona 93.
ìKaratasi za mtihani wa watahiniwa wenye mahitaji maalum zimeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji yao kama vile kutumia karatasi za maandishi yenye nundu kwa wasioona na kuongeza ukubwa wa maandishi kwa wenye uoni hafifu,î alisema.
Mchome alisema umuhimu wa mtihani huo ni kupima kiwango cha maarifa na ujuzi alioupata mwanafunzi kutokana na mada alizojifunza katika kidato cha kwanza na cha pili.
Pia alisema mtihani huo unatoa changamoto zinazosaidia wanafunzi, walimu, wizara na wadau wa elimu kutambua mapungufu yaliyopo katika ufundishaji ili yaweze kufanyiwa marekebisho kwa lengo la kuboresha elimu.www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company